Al-Israa
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَٱسْتَفْزِزْ مَنِ ٱسْتَطَعْتَ مِنْهُم بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِم بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِى ٱلْأَمْوَٰلِ وَٱلْأَوْلَـٰدِ وَعِدْهُمْ ۚ وَمَا يَعِدُهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ إِلَّا غُرُورًا 64
{64} Kisha Mwenyezi Mungu akamwamuru afanye kila awezalo katika kuwapoteza, akasema, "Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako" na anaingia katika hili kila anayelingania katika maasia. "Na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu." Na inaingia katika hili kila mpandaji na mtembeaji katika kumuasi Mwenyezi Mungu. Basi yeye ni miongoni mwa jeshi lake la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Kinachokusudiwa ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwajaribu waja wake kwa adui huyu wa wazi anayewalingania katika kumuasi Mwenyezi Mungu kwa maneno yake na matendo yake. "Na shirikiana nao katika mali na wana." Haya yanajumuisha kila dhambi linalohusiana na mali yao na watoto wao, kama vile kukataa kutoa zaka, fidia mbalimbali, na haki za faradhi, kutowapa adabu nzuri watoto na kuwalea katika heri na kuacha maovu, kuchukua mali bila ya haki au kuitumia kwa yasiyo ya haki, au kutumia mapato mabaya. Basi wengi katika wafasiri walitaja kuwa hilo kumshirikisha Shetani katika mali na watoto, kunajumuisha kuacha kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula, kunywa, au kufanya tendo la ndoa, na kwamba ikiwa hatalitaja jina la Mwenyezi Mungu katika hayo, basi Shetani atashirikiana naye, kama ilivyokuja katika Hadithi. "Na waahidi" ahadi za uongo ambazo hazina uhakika wowote. Na ndiyo maana akasema, "Na Shetani hawapi ahidi isipokuwa ya udanganyifu" yenye kupotelea mbali, kama vile kuwapambia maasia na itikadi potovu, na akawaahidi malipo juu yake, kwa sababu wanadhani kwamba wako katika haki. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, “Shetani anawatia hofu ya ufukara na anawaamrisha mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anawaahidi msamaha na fadhila zitokazo kwake."