Yusuf
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
قَالَ هِىَ رَٰوَدَتْنِى عَن نَّفْسِى ۚ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّنْ أَهْلِهَآ إِن كَانَ قَمِيصُهُۥ قُدَّ مِن قُبُلٍ فَصَدَقَتْ وَهُوَ مِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ 26
{26} Basi Yusuf akajiweka mbali na yale aliyomsingizia, na "akasema: Yeye ndiye aliyenitaka bila ya mimi kumtaka" kwa hivyo kufikia hapo hali ya kila mmoja wao ikawa na uwezekano wa kuwa ndiyo ya ukweli, wala hakujua ni nani kati yao, isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiwekea haki na ukweli ushahidi mbalimbali na alama zinazoyaashiria, ambazo waja Wake wanaweza kuzijua au wasiweze kuzijua. Na katika suala hili Mwenyezi Mungu Mtukufu alineemesha kwamba ajulikane mkweli kati yao ili kumuondoa hatiani Nabii Wake na mteule wake, Yusuf, amani iwe juu yake. Kwa hivyo, akajitokeza shahidi kutoka kwa familia yake mwanamke huyo akatoa ushahidi kwa uthibitisho ambao mwenye kupatikana nao ndiye mkweli. Kwa hivyo akasema: "Ikiwa shati lake limechanwa kwa mbele, basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo." Kwa sababu hilo linaashiria kuwa yeye ndiye aliyemjia, aliyemtaka, aliyemshambulia, na kwamba mwanamke huyo alitaka kumsukuma amuondokee, kwa hivyo akalirarua shati lake kutokea upande huu.