Yusuf
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَرَٰوَدَتْهُ ٱلَّتِى هُوَ فِى بَيْتِهَا عَن نَّفْسِهِۦ وَغَلَّقَتِ ٱلْأَبْوَٰبَ وَقَالَتْ هَيْتَ لَكَ ۚ قَالَ مَعَاذَ ٱللَّهِ ۖ إِنَّهُۥ رَبِّىٓ أَحْسَنَ مَثْوَاىَ ۖ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ 23 وَلَقَدْ هَمَّتْ بِهِۦ ۖ وَهَمَّ بِهَا لَوْلَآ أَن رَّءَا بُرْهَـٰنَ رَبِّهِۦ ۚ كَذَٰلِكَ لِنَصْرِفَ عَنْهُ ٱلسُّوٓءَ وَٱلْفَحْشَآءَ ۚ إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُخْلَصِينَ 24
Mtihani huu mkubwa ni mkubwa zaidi kwa Yusuf kuliko mtihani wa ndugu zake, na subira yake juu yake kuna malipo makubwa zaidi kwa sababu kusubiri kwa hiari licha ya kuwepo kwa sababu nyingi za kufanya kitendo hicho. Kwa hivyo, akatanguliza upendo wa Mwenyezi Mungu mbele ya hilo. Na ama mtihani wake kutoka kwa ndugu zake, huo kusubiri juu yake ni subira ya lazima, ambao ni kama maradhi na machukizo ambayo humsibu mja bila ya hiyari yake, na wala hana pa kukimbilia isipokuwa kuwa tu na subira juu yake, kwa kutii au kuchukia.
{23-24} Haya ni kwa sababu Yusuf, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alibaki mwenye kuheshimiwa katika nyumba ya yule mheshimiwa, na alikuwa na uzuri, na ukamilifu, na urembo kiasi kwamba ilimlazimu kwamba, "Na yule bibi wa nyumba aliyokuwamo Yusuf akamtamani kinyume cha nafsi yake." Yaani, alikuwa mtumishi wake na alikuwa chini ya uendeshaji wake, na maskani yalikuwa mamoja ambapo ilikuwa rahisi kwake kutekeleza jambo la kuchukiza bila kutambuliwa na yeyote wala kuhisiwa na mwanadamu yeyote. "Na" msiba huo ukazidi kwa sababu "alifungafunga milango" na mahali pale pakawa tupu, na wakasalimika kutokana na mtu yeyote kuwaingilia kwa sababu milango ilikuwa imefungwa. Na bibi huyo alikuwa amemuita kwa nafsi yake, akasema: "Njoo!" Yaani, fanya jambo linalochukiza na uje kwangu! Na pamoja na hayo alikuwa mgeni ambaye hawezi kuwa na adabu kama ile angekuwa nayo katika nchi yake na miongoni mwa wale wanaomjua, na alikuwa mfungwa chini ya mkono wake, na mwanamke huyo alikuwa bibi yake, naye alikuwa mzuri unaoita kile kilichoko huko, naye alikuwa barobaro mseja, na alikuwa amemtishia iwapo hatafanya alichomuamrisha kuwa atafungwa jela au adhabu chungu. Lakini akawa na subira katika kutomuasi Mwenyezi Mungu pamoja na kuwepo sababu yenye nguvu ya kufanya hivyo ndani yake. Kwa sababu alikuwa ameazimia juu yake azimio ambalo aliliacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akayatanguliza matashi ya Mwenyezi Mungu mbele ya matashi ya nafsi yenye kuamrisha mabaya, na akaona katika ushahidi wa Mola wake Mlezi - ambao ni elimu aliyokuwa nayo na imani ambayo yalimlazimu kujieka mbali na kuacha maasia haya makubwa Mwenyezi na "Yusuf akasema: Audhubillahi (Najikinga na Mwenyezi Mungu!)" Yaani, najikinga kwa Mwenyezi Mungu kufanya kitendo hiki kibaya. Kwa sababu ni katika mambo yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu na kumtenga mtu naye, na kwa sababu ni hiyana dhidi ya bwana wangu, ambaye aliniweka maskani mazuri. Basi hainifailii nimkabili katika mkewe kwa mkabala mbaya zaidi, na hii ni katika dhuluma kubwa zaidi, na dhalimu hafaulu. Na muhtasari wa hayo ni kwamba aliweka vizuizi dhidi ya yeye kufanya kitendo hiki: kumcha Mungu, kuzingatia haki za bwana wake aliyemkirimu, na kujitunza dhidi ya dhuluma ambayo hafaulu mwenye kujihusisha nayo, na pia uthibitisho wa imani ambao Mwenyezi Mungu alimneemesha nao ambao uko moyoni mwake, ilimtaka kutekeleza maamrisho na kuepuka makemeo. Na chenye kukusanya hayo yote ni kwamba, Mwenyezi Mungu alimwondolea ubaya huo na uchafu, kwa sababu yeye ni miongoni mwa waja Wake ambao wanamfanyia yeye tu ibada zao; ambaye Mwenyezi Mungu aliwasafisha, na akawachagua na akawafanya kuwa kwa ajili Yake tu; na akawaneemesha kwa neema mbalimbali, na akawaepusha na machukizo ambayo kwayo wakawa katika bora zaidi wa viumbe Wake.