İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Hud
Sure 11

Hud

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 14

فَإِلَّمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَكُمْ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَآ أُنزِلَ بِعِلْمِ ٱللَّهِ وَأَن لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ 14

{14} "Na wasipowaitikia" juu ya lolote katika hayo, "basi jueni ya kwamba (Qur-ani hii) imeteremshwa kwa elimu ya Mwenyezi Mungu" kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu, ushahidi unaohitaji hilo ulikwisha simama, na kizuizi kwamba hakuna upinzani wowote juu ya hilo, "na kwamba hakuna mungu isipokuwa Yeye." Yaani, jueni kwamba hakuna mungu isipokuwa Yeye. Yaani, Yeye peke yake ndiye anayestahiki uungu na kuabudiwa. "Basi je, nyinyi ni Waislamu?" Yaani, mmefuata uungu Wake, kujisalimisha kwa uja kwake. Katika aya hizi kuna mwongozo kwamba mwenye kulingania kwa Mwenyezi Mungu hafai kuzuiliwa na pingamizi za wale wanaompinga au kashfa za wanaomkosoa, hasa ikiwa kashfa hiyo haina msingi wowote, na haitii doa katika kile anachokiitia. Na kwamba, moyo wake usiwe na dhiki, bali atulie na hilo, na aendelee na jambo lake, na aelekee kwa mambo yake. Na kwamba, si lazima kuitikia mapendekezo ya wanaopendekeza kwa ushahidi wanaouchagua wao. Bali inatosha tu kusimamisha ushahidi ulio salama kutokana na upinzani wowote juu ya masuala na madai yote. Na ndani yake kuna kwamba Qur-ani hii ni muujiza yenyewe. Kwa sababu, hakuna yeyote anayeweza kuleta mfano wake wala sura kumi mfano wake, bali sura moja mfano wake. Kwa sababu, maadui wenye usemi bora zaidi na ufasaha, Mwenyezi Mungu aliwapa changamoto ya kufanya hivyo, lakini hawakumpinga. Kwa sababu, walijua kwamba hawana uwezo wa kufanya hivyo. Na ndani yake kuna kwamba, miongoni mwa mambo ambayo elimu yake inatafutwa na kwamba kuna tu na dhana kubwa ju yake haitoshi, ni elimu ya Qur-ani na elimu ya tauhidi. Kwa sababu ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, "basi jueni ya kwamba, (Qur-ani hii) imeteremshwa kwa elimu ya Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna mungu isipokuwa Yeye."