İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yunus
Sure 10

Yunus

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 94

فَإِن كُنتَ فِى شَكٍّ مِّمَّآ أَنزَلْنَآ إِلَيْكَ فَسْـَٔلِ ٱلَّذِينَ يَقْرَءُونَ ٱلْكِتَـٰبَ مِن قَبْلِكَ ۚ لَقَدْ جَآءَكَ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُمْتَرِينَ 94

{94} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: -"Na ikiwa uko katika shaka juu yale tuliyokuteremshia" je ni sahihi au si sahihi, "basi waulize wale wasomao Kitabu kabla yako." Yaani, waulize watu wa Vitabu waadilifu, na wanazuoni wenye msingi madhubuti. Kwa maana, wao hakika watakukiria ukweli wa yale ambayo yalijulisha na kuafikiana kwake na yale waliyo nayo. Na ikisemwa: Hakika Wengi katika Watu wa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Manasara, na pengine wengi wao walikuwa wamemkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wakampinga, na wakaukataa wito wake. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwamrisha Mtume wake awafanye kuwa mashahidi, na akaufanya ushahidi wao kuwa hoja juu ya yale aliyokuja nayo, na ushahidi juu ya usahihi wake. Basi linawezaje kuwa hivyo? Jibu la hili ni kwa namna mbalimbali: Miongoni mwake ni kwamba, ushahidi unapofungamanishwa na kundi au watu wa dhehebu fulani au mji fulani na mfano wao, basi huo unajumuisha watu waadilifu wakweli miongoni mwao. Na ama wasiokuwa wao, hata kama wao ndio wengi miongoni mwao, basi hao hawazingatiwi. Kwa maana, ushahidi umejengeka juu ya uadilifu na ukweli, na hilo tayari lilikwisha patikana katika kuamini kwa wengi wa marabi wao wamuabuduo Mola wao Mlezi tu, kama vile 'Abdullah bin Salam na wenzake, na wengi miongoni mwa wale waliosilimu katika wakati wa Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – na makhalifa wake baada yao. Na miongoni mwake ni kwamba, Ushahidi wa Watu wa Kitabu kwa Mtume umejengeka juu ya kitabu chao, Taurati, ambayo wao wanajinasibisha nayo. Basi ikiwa kuna yale yanayoafikiana na Qur’an katika Taurati, na yanaisadikisha, na yanaishuhudia kuwa ni ukweli, basi hata kama wataafikiana tangu wa mwanzo wao hadi wa mwisho wao juu ya kulikataa hilo, basi hilo halitatia doa katika yale aliyokuja nayo Mtume. Na miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwamrisha Mtume wake kutafuta ushahidi wa Watu wa Kitabu juu ya usahihi wa yale yaliyomjia, na akalidhihirisha hilo na akaliweka hadharani mbele ya mashahidi hao. Na inavyojulikana ni kwamba wengi wao walikuwa miongoni mwa watu wenye pupa zaidi juu ya kubatilisha wito wa Mtume Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - na lau wangelikuwa na cha kukanusha yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu, basi wangelikifichua, na kukidhihirisha, na kukibainisha. Lakini kwa kuwa hakukuwa na lolote kati ya hayo lililotokea, basi kukawa kutopinga kwa wapinzani, na maadui, na kukiri kwa anayepaswa kujibu, ni miongoni mwa ushahidi mkubwa zaidi juu ya usahihi na Qur-ani hii na ukweli wake. Na miongoni mwake ni kwamba, si wengi wa Watu wa Kitabu waliokataa wito wa Mtume, bali wengi wao waliuitikia na kuufuata kwa kujitolea na kwa hiari. Kwa maana, Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alitumwa kama Mtume ilhali wengi wa watu wa ardhi wenye dini ni Watu wa Kitabu, na Dini yake haikudumu kwa muda mrefu mpaka wakaifuata watu wengi wa Shaam, Misri, Iraqi na nchi jirani ambazo ndiyo makao ya Dini ya Watu wa Kitabu. Na wala hawakubakia isipokuwa watu wa uongozi tu ambao walipendelea uongozi wao kuliko haki na wale waliowafuata miongoni mwa watu wa kawaida wasiojua, wale waliowafuata dini yao kwa jina tu, si kwa kimaana, kama vile Wafrank, ambao ukweli wao ni kwamba wao ni watu wasiopenda dini ambao wamezikana dini zote za Mitume, bali wamejihusisha na dini ya Kikristo ili kuendeleza ufalme wao na kuficha uwongo wao. Hii pia inajulikana na wale wanaojua hali zao wazi na zinazoonekana. Na kauli yake: "Kwa yakini imekwisha kujia haki," yaani, ambayo haina shaka yoyote ndani yake kwa namna yoyote ile, "kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe kabisa miongoni mwa wenye shaka." Kama kauli yake Yeye Mtukufu, "Kitabu kilichoteremshwa kwako, basi isiwe dhiki yoyote katika kifua chako kwa sababu yake."