Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 98 · Aya ya 2

Al-Bayyina 98:2

البينة

رَسُولٌ مِّنَ ٱللَّهِ يَتْلُوا۟ صُحُفًا مُّطَهَّرَةً

Maana

Yaani Mtume aliyetoka kwa Mwenyezi Mungu anayewasomea kurasa zilizotakasika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika! [2]

[2] Na hoja hiyo ni Mtume aliye tumwa kutokana na Mwenyezi Mungu awasomee kurasa zilizo takasika na upotovu,

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na alama hiyo ni Mtume wa Allah Mtukufu, Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), mwenye kuwasomea Qur’ani iliyomo kwenye kurasa zilizo safi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Bayyina

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net