Al-Bayyina 98:1
البينةلَمْ يَكُنِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ وَٱلْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ ٱلْبَيِّنَةُ
Hawakuwa waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache waliyo nayo mpaka iwajie bayana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana! [1]
[1] Hawakuwa walio mkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake miongoni mwa Mayahudi na Wakristo, na miongoni mwa washirikina, waache kughafilika kwao na ujinga wao kuto ijua Haki mpaka iwajie hoja ya kukata.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haikua kwa wenye kukufuru miongoni mwa mayahudi na manaswara na washirikina ni wenye kuacha ukafiri wao isipokua mpaka iwajie alama walioahidiwa katika vitabu vilivyopita, yani walikua wanadai kua wakiona hiyo alama wataamini, lakini wakageuka isipokua wachache.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net