At-Tawba 9:86
التوبةوَإِذَآ أُنزِلَتْ سُورَةٌ أَنْ ءَامِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَجَـٰهِدُوا۟ مَعَ رَسُولِهِ ٱسْتَـْٔذَنَكَ أُو۟لُوا۟ ٱلطَّوْلِ مِنْهُمْ وَقَالُوا۟ ذَرْنَا نَكُن مَّعَ ٱلْقَـٰعِدِينَ
Na inapoteremshwa sura kwamba muaminini Mwenyezi Mungu na piganeni Jihadi pamoja na Mtume wake, wale wenye nguvu miongoni mwao hukutaka ruhusa na wanasema: Tuache tuwe pamoja na wanaokaa nyuma!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na inapo teremshwa Sura isemayo: Muaminini Mwenyezi Mungu na piganeni Jihadi pamoja na Mtume wake, wale wenye nguvu miongoni mwao hukutaka ruhusa na husema: Tuache tuwe pamoja na wanao kaa nyuma! [86]
[86] Na hawa wanaafiki wakisikia chochote ulicho teremshiwa katika Qur'ani kinacho wataka wamsafie Imani Mwenyezi Mungu, na wende kwenye Jihadi pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, matajiri na wenye nguvu katika wao wanakutaka uwaachilie wasende nawe kwenye Jihadi, na husema: Tuache tuwe na hawa walio pewa ruhusa kukaa nyuma Madina.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na pindi sura yoyote ikiteremshwa kwa Muhammad (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), inayoamrisha kumuamini Allah Mtukufu na kumtakasa na kupigana jihadi pamoja na Mtume wa Allah Mtukufu, wale wenye uwezo wa kifedha miongoni mwa wanafiki wanakuomba ruhusa na wanasema, «Tuache pamoja na waliokaa wasioweza kutoka».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net