Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 85

At-Tawba 9:85

التوبة

وَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَٰلُهُمْ وَأَوْلَـٰدُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُعَذِّبَهُم بِهَا فِى ٱلدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَـٰفِرُونَ

Maana

Wala zisikupendeze mali zao na watoto wao. Hakika Mwenyezi Mungu anataka tu kuwaadhibu kwa hayo katika dunia; na zitoke roho zao hali ya kuwa ni makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala zisikushitue mali zao na watoto wao. Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwa hayo katika dunia; na zitoke roho zao na hali wao ni makafiri. [85]

[85] Wala usistaajabu, ewe Mtume, kuona tulivyo wapa mali na wana, juu ya kuwa tumeudhika nao. Hayakuwa hayo kwa kuwa tunawapendelea wao zaidi, lakini ni kutekeleza anayo yataka Mwenyezi Mungu yawapate, nayo ni shakawa ya duniani kwa kushughulikia kukusanya mijimali tu pamoja na yaliyo lazimikana nayo. Nayo ni hizo hamu na masaibu yanayo ambatana na ukusanyaji wa mali. Na ili yatimie anayo yataka Mwenyezi Mungu yawe, nayo ni kuwa waifariki dunia nao ni makafiri, iwe wamekhasiri dunia na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na zisikushangaze mali za wanafiki hawa na watoto wao. Allah Mtukufu Anataka kuwaadhibu wao kwa hizo ulimwenguni, kwa kupambana kwao na shida katika kuzipata na kwa kufa kwao katika hali ya kumkanusha Allah Mtukufu na Mtume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net