At-Tawba 9:121
التوبةوَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً وَلَا يَقْطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ ٱللَّهُ أَحْسَنَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Wala hawatoi masurufu madogo wala makubwa, wala hawalivuki bonde, isipokuwa huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu awalipe bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala hawatoi cha kutoa kidogo wala kikubwa, wala hawalivuki bonde, ila huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyo kuwa wakiya- tenda. [121]
[121] Na kadhaalika Mujaahidina hawatoi mali wanayo toa, kingi na kidogo, wala hawasafiri safari yoyote, kwa Njia ya Mwenyezi Mungu ila huandikiwa katika madaftari ya vitendo vyao vyema, ili wapate malipo wanayo stahiki kuyapata hao watendao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wala hawatoi matumizi, madogo au makubwa, katika njia ya Allah Mtukufu, wala hawayapiti mabonde katika kutembea kwao pamoja na Mtume wa Allah Mtukufu (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye), katika kupigana kwake jihadi, isipokuwa wataandikiwa thawabu ya tendo lao, ili Allah Mtukufu Awalipe mazuri zaidi ya wao kulipwa kwa matendo yao mema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net