Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 120

At-Tawba 9:120

التوبة

مَا كَانَ لِأَهْلِ ٱلْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ ٱلْأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُوا۟ عَن رَّسُولِ ٱللَّهِ وَلَا يَرْغَبُوا۟ بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِۦ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَطَـُٔونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ ٱلْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِۦ عَمَلٌ صَـٰلِحٌ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ ٱلْمُحْسِنِينَ

Maana

Haiwafailii watu wa Madina na Mabedui walio kando kando yao kusalia nyuma wasitoke pamoja na Mtume, wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake. Hayo ni kwa sababu wao hakiwapati kiu, wala machovu, wala njaa, katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaendi mahali panapowaghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, isipokuwa huandikiwa kwa hicho kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya uzuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio jirani zao kubakia nyuma wasitoke na Mtume, wala kujipendelea nafsi zao kuliko yeye. Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa, kwa ajili ya Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapo waghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kuwa ni kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanao fanya mema. [120]

[120] Haikuwa ni halali kwa wakaazi wa Madina na majirani zao katika wakaazi wa majangwani kubaki nyuma wasitoke kwenda vitani pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. Wala kujifanyia uchoyo kwa ajili ya nafsi zao katika aliyo jitolea Mtume nafsi yake. (Mtume kajitolea roho na mali kwa kupigania Haki.) Kwani wao hakiwapati, katika Njia ya Mwenyezi Mungu, kiu, au machofu, au njaa, wala hawashuki pahala panapo watia ghadhabu makafiri, wala hakiwasibu kutokana na adui chochote kama kushindwa au kunyan'ganywa ngawira, ila huhisabiwa kwa hayo yote kuwa ni a'mali njema, ya kulipiwa bora ya malipo. Na Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wenye kufanya mema katika vitendo vyao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Haikuwa inafaa kwa watu wa mji wa Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na walio pembezoni mwao miongoni mwa wanaokaa jangwani, kujikalisha nyuma pamoja na watu wao majumbani mwao na kuacha kumfuata Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukiye). Na haikuwa inafaa kwao kuzipendelea nafsi zao mapumziko huku Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), yuko kwenye tabu na usumbufu. Hayo ni kwamba wao hawapatikani na kiu wala usumbufu wala njaa kwenye safari yao na jihadi yao katika njia ya Allah Mtukufu, na wala hawakanyagi ardhi yoyote ambayo kuikanyaga kwao inawatia hasira makafiri, na wala hawafaulu kumuua au kumshinda adui wa Allah Mtukufu na adui wao isipokuwa wataandikiwa, kwa hayo yote, thawabu ya tendo jema. Hakika Allah Mtukufu Hapotezi malipo ya muhsinûn: waliofanya wema kwa kukimbilia kwao kufuata amri ya Allah Mtukufu na kusimama kwao imara kutekeleza haki Yake inayowalazimu na haki ya viumbe Vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net