Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 11

At-Tawba 9:11

التوبة

فَإِن تَابُوا۟ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُا۟ ٱلزَّكَوٰةَ فَإِخْوَٰنُكُمْ فِى ٱلدِّينِ ۗ وَنُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ

Maana

Kwa hivyo wakitubu, na wakasimamisha Sala, na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na tunazipambanua Aya kwa kaumu wanaojua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi wakitubu na wakashika Swala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na tunazichambua Aya kwa watu wajuao. [11]

[11] Wakitubia, wakaacha ukafiri wao, na wakashika hukumu za Uislamu, kwa kushika Swala, na kutoa Zaka, basi wanakuwa ni ndugu zenu katika Dini. Haki yao kama haki yenu. Jukumu lao kama jukumu lenu. Na Mwenyezi Mungu anazibainisha Aya hizi kwa watu wanao nafiika na ilimu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na iwapo watakomeka na ibada ya asiyekuwa Allah Mtukufu, wakalitamka neno la kumpwekesha, wakajilazimisha na sheria za Kiislamu za kusimamisha Swala na kutoa Zaka, basi hao ni ndugu zenu katika Uislamu. Na tunazieleza waziwazi aya na kuzifafanua kwa watu wenye kufaidika nazo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net