At-Tawba 9:10
التوبةلَا يَرْقُبُونَ فِى مُؤْمِنٍ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُعْتَدُونَ
Hawachungi kwa Muumini udugu wala ahadi. Basi hao ndio wapindukiao mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hawatazami kwa Muumini udugu wala ahadi; basi hao ndio warukao mipaka. [10]
[10] Hiyo ndiyo hali ya ukafiri wao. Hawahishimu ujamaa wala ahadi katika kuamiliana na Muumini. Shani ya watu kama hao ni kufanya uadui tu. Hayo ndiyo maradhi yao yasio wabanduka!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Washirikina hawa wako kwenye vita dhidi ya Imani na watu wake, hawaupi uzito wowote ujamaa wa Muumini wala mapatano yake; walilonalo wao ni uadui na udhalimu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net