Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 84 · Aya ya 25

Al-Inshiqaaq 84:25

الإنشقاق

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍۭ

Maana

Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usiomalizika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika. [25]

[25] Lakini walio amini na wakatenda mema watapata, kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ujira usio wakatikia na wala usio kuwa na hisabu juu yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lakini wale wanaomuamini Allah Mtukufu na Mtume wake na wakatekeleza amri waliyofaradhiwa na Allah Mtukufu watakuwa na malipo, Siku ya Akhera, yasiyokatika wala kupungua.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Inshiqaaq

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net