Al-Inshiqaaq 84:15
الإنشقاقبَلَىٰٓ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرًا
Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona vyema!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona! [15]
[15] Bali atarejea, na atahisabiwa! Kwani Mola wake Mlezi alikuwa anamwona vyema yeye na vitendo vyake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sivyo hivyo! Allah Mtukufu Atamrudisha kama alivomuumba na kumlipa kwa amali zake. Kwani Yeye kwake ni Mtambuzi, na kwa hali yake ni Mjuzi, kuanzia Alipomuumba mpaka kumfufua.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net