Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 82 · Aya ya 6

Al-Infitaar 82:6

الإنفطار

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْإِنسَـٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلْكَرِيمِ

Maana

Ewe mwanadamu! Nini kilichokudanganya ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? [6]

[6] Ewe mwanaadamu! Kitu gani kilicho kukhadaa wewe na Mola wako Mlezi Mtukufu hata ukafanya jeuri ya kwenda kumuasi? (Ni dhaahiri kuwa Sayyid Abdulla bin Ali bin Nassir aliye tunga utenzi wa Kiswahili maarufu uitwao Al Inkishaf aliiwaza Aya hii alipo tunga ubeti huu: Moyo wangu nini huzundukani Likughurielo hela ni nni? Hunelezi nami kalibaini Liwapo na sura nisikataye )

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe binadamu unayekanusha kufufuliwa! Ni kipi kilichokufanya uhadaike na ughurike kuhusu Mola wako Mpaji Mwenye kheri nyingi, Anayestahiki kushukuriwa na kutiiwa?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Infitaar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net