Al-Insaan 76:8
الانسانوَيُطْعِمُونَ ٱلطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا
Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. [8]
[8] Na huwalisha chakula mafakiri wasio weza kazi, na watoto walio fiwa na wazee wao, na wafungwa wasio miliki kitu, ijapo kuwa wao wenyewe hao watoaji wanakipenda hicho wanacho kitoa, na wanakihitajia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanalisha chakula, pamoja na kuwa wanakipenda na kukihitajia, humpa chakula hicho fukara asiyeweza kuchuma, asiyemiliki chochote katika vitu vya kilimwengu, na humpa mtoto aliyefiliwa na babake kabla ya kubaleghe na asiye na mali, na humpa mtu aliyetekwa vitani miongoni mwa washirikina na wengineo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net