Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 76 · Aya ya 7

Al-Insaan 76:7

الانسان

يُوفُونَ بِٱلنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُۥ مُسْتَطِيرًا

Maana

Wanatimiza nadhiri, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana, [7]

[7] Wanatekeleza yaliyo wajibikia , na wanaikhofu Siku kubwa hiyo ambayo madhara yake yataenea kote kote,

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao walikuwa huko duniani wanatekeleza kile walichojilazimisha nafsi zao cha utiifu kwa Allah Mtukufu, na wakiogopa mateso ya Allah Mtukufu, Siku ya Kiyama, ambayo madhara yake ni hatari, na ubaya wake ni wenye kusambaa na kuenea kwa watu, isipokuwa wale ambao Allah Mtukufu Amewarehemu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Insaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net