Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 76 · Aya ya 29

Al-Insaan 76:29

الانسان

إِنَّ هَـٰذِهِۦ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا

Maana

Hakika haya ni mawaidha; basi anayetaka, atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi. [29]

[29] Hakika Sura hii ni mawaidha kwa walimwengu wote. Basi mwenye kutaka atafuata njia ya Imani na uchamngu kwendea kwa Mola wake Mlezi imfikishe kwenye maghfira yake na Pepo yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika ndani ya sura hii, kwa yaliyomo ya kuvutia na kuogopesha, ya kuahidi mema na kuonya mabaya, kuna mawaidha kwa viumbe wote. Basi mwenye Kuitakia mema nafsi yake duniani na Akhera, na ashike njia ya Imani na uchamungu, itakayomfikisha kwenye msamaha wa Allah Mtukufu na radhi Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Insaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net