Al-Insaan 76:12
الانسانوَجَزَىٰهُم بِمَا صَبَرُوا۟ جَنَّةً وَحَرِيرًا
Na atawalipa Bustani za mbinguni na maguo ya hariri kwa vile walivyosubiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri. [12]
[12] Na akawajazi kwa ile subira yao Pepo imeenea furaha, na nguo zake ni hariri laini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Atawalipa, kwa kuvumilia kwao duniani juu ya utiifu, Pepo iliyo kubwa ambayo ndani yake watakula wanachokitaka na watavaa humo hariri laini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net