Al-Insaan 76:11
الانسانفَوَقَىٰهُمُ ٱللَّهُ شَرَّ ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمِ وَلَقَّىٰهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا
Basi Mwenyezi Mungu atawalinda kutokana na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi Mwenyezi Mungu atwalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha. [11]
[11] Basi Mwenyezi Mungu akawalinda na shida za siku hiyo, na badala ya mkunjo wa wenye maasi, akawapa nyuso za kupendeza, na ukunjufu na furaha katika nyoyo zao,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi hao Allah Mtukufu Atawaokoa na shida za Siku hiyo, na Atawapa uzuri na nuru katika nyuso zao, na furaha ndani ya nyoyo zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net