Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 88

Al-A'raaf 7:88

الأعراف

قَالَ ٱلْمَلَأُ ٱلَّذِينَ ٱسْتَكْبَرُوا۟ مِن قَوْمِهِۦ لَنُخْرِجَنَّكَ يَـٰشُعَيْبُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَكَ مِن قَرْيَتِنَآ أَوْ لَتَعُودُنَّ فِى مِلَّتِنَا ۚ قَالَ أَوَلَوْ كُنَّا كَـٰرِهِينَ

Maana

Wakasema waheshimiwa waliotakabari katika kaumu yake, "Lazima tutakutoa ewe Shu'aib na wale walioamini pamoja nawe katika mji wetu, au lazima mtarejea katika mila yetu." Akasema, "Je, hata kama tunachukia?"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

WAHESHIMIWA WALIO TAKABARI katika kaumu yake wakasema: Ewe Shua'ib! Tutakutoa wewe pamoja na wale walio kuamini katika mji wetu, au mrejee katika mila yetu. Akasema: Je, ingawa tunaichukia? [88]

[88] Hii ni khabari ya Shua'ib katika wito wake kuwalingania kaumu yake. Ama hao kaumu yake walikuwa wamemili juu ya upotovu. Na wale wakubwa wao walio takabari waliukataa wito, na wakaona ni uvunjifu kuifuata Haki. Wakamkabili Shua'ib kumwambia dhamiri yao kwa kusema: Hakika hapana vingine ila tukutoe wewe na hao walio amini pamoja nawe katika mji wetu. Na tutakufukuzeni, wala hamtasalimika na adhabu hii ila mkirejea katika hii dini yetu mliyo iacha. Shua'ib a.s. akawajibu kwa kusema: Turejee katika mila yenu na hali sisi tunaichukia kwa uharibifu wake? Hayawi hayo abadan!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walisema wakubwa wa watu wa Shu‛ayb waliokataa, kwa kiburi, kumuamini Allah Mtukufu na kumfuata Mtume Wake Shu‛ayb, amani imshukiye, «Tutakutoa, ewe Shu‛ayb, wewe na walio pamoja na wewe kutoka kwenye miji yetu, isipokuwa ukiwa utarudi kwenye dini yetu.» Shu‛ayb akasema akilipinga na kulionea ajabu neno lao, «Je, tuwafuate nyinyi kwenye dini yenu na mila yenu ya batili hata kama sisi tunaichukia kwa kujua kwetu ubatili wake?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net