Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 85

Al-A'raaf 7:85

الأعراف

وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۗ قَالَ يَـٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُۥ ۖ قَدْ جَآءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ فَأَوْفُوا۟ ٱلْكَيْلَ وَٱلْمِيزَانَ وَلَا تَبْخَسُوا۟ ٱلنَّاسَ أَشْيَآءَهُمْ وَلَا تُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَـٰحِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Maana

Na kwa (watu wa) Madyana tulimtuma ndugu yao Shu'aib. Akasema, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Hamna mungu yeyote isipokuwa Yeye. Hakika imekwishawajia hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi timizeni sawasawa vipimo na mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika ardhi baada ya kutengenea kwake. Hayo ndiyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Hamna mungu mwengine isipo kuwa Yeye. Imekwisha kufikieni hoja wazi kutoka kwa Mola Mlezi wenu. Basi timizeni sawasawa vipimo na mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika nchi, baada ya kuwa imekwisha tengenea. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini. [85]

[85] Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yao, Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake. Kwani nyinyi hamna mungu isipo kuwa Yeye. Hoja zilizo wazi za kuthibitisha Haki inayo toka kwa Mola Mlezi wenu juu ya Utume wangu kwenu zimekwisha kujieni. Na umekujieni Ujumbe wa Mola wenu Mlezi kwamba mtengeneze kwa uadilifu maingiliano yenu nyinyi kwa nyinyi. Basi timizeni vipimo na mizani mnapo uziana, wala msipunguze haki za watu, wala msiiharibu nchi nzuri, kwa kufisidi mapando na kadhaalika, na kuwatenga jamaa na kuondoa mapenzi. Kwani hayo ni bora kwenu mkiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mnaamini Haki iliyo wazi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tulimtuma, kwa watu wa kabila linalokaa Madyan, ndugu yao Shu‛ayb, amani imshukie, akasema kuwaambia, Enyi wtu wangu, muabuduni Allah Mtukufu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Hamna mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu. Mtakasieni ibada.Hakika imewajia nyinyi hoja, kutoka kwa Mola wenu, juu ya ukweli wa yale ninayowaitia. Watekelezeeni watu haki zao kwa kutimiza vipimo na mizani. Na msiwapunguzie haki zao mkawadhulumu. Wala msifanye uharibifu katika ardhi, kwa ukafiri na kudhulumu, baada ya kuwa imetengenezwa kwa sheria za Mitume waliopita, amani iwashukie. Hayo niliyowaitia nyinyi ni bora kwenu katika ulimwengu wenu na Akhera yenu, iwapo nyinyi ni wenye kuniamini katika yale ninayowaitia, ni wenye kuzifuata sheria za Allah Mtukufu kivitendo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net