Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 84

Al-A'raaf 7:84

الأعراف

وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُجْرِمِينَ

Maana

Na tukawanyeshea mvua. Basi tazama jinsi ulivyokuwa mwisho wa wahalifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukawamiminia mvua. Basi tazama jinsi ulivyo kuwa mwisho wa wakosefu. [84]

[84] Basi tuliwateremshia mvua ya mawe ya kuteketeza, na ardhi ikatandazwa kwa mitetemeko ya chini yao! Basi ewe Nabii! Angalia vipi ulikuwa mwisho wa wakosefu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Akawaadhibu makafiri wa kaumu ya Lût, kwa kuwateremshia wao mvua ya mawe, Akaigeuza nchi yao Akaifanya juu ni chini na chini ni juu. Tazama ulivyokuwa mwisho wa wale waliojasiri kufanya matendo ya kumuasi Allah Mtukufu na wakawakanusha Mitume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net