Al-A'raaf 7:82
الأعرافوَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓا۟ أَخْرِجُوهُم مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ
Na halikuwa jibu la kaumu yake isipokuwa walisema, "Watoeni kutoka katika mji wenu. Maana wao hakika ni watu wanaojitakasa."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na haikuwa jawabu ya kaumu yake isipo kuwa kuambizana: Wafukuzeni katika mji wenu, maana hao ni watu wanao jitakasa. [82]
[82] Na haikuwa jawabu ya watu wake kwa kukatazwa hichi kitendo kiovu kisicho kuwa na mfano, ila ni kusema: Watoeni Lut' na jamaa zake na wafuasi wake katika mji wenu! Nayo ni kwa kuwa wao wanajitahirisha na wanajitenga na hichi kitendo ambacho akili na maumbile yanakiona ni kibaya, na wao hao watu wanakioni kizuri!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hayakuwa majibu ya watu wa Lût, alipowapinga kwa kitendo chao kilichofikia upeo wa ubaya, isipokuwa ni kuambiana wao kwa wao, «Mtoeni Lût na wafuasi wake nchini mwenu, kwa kuwa yeye na wanaomfuata ni watu wanaojiepusha na kuwajia wanaume kwenye sehemu zao za nyuma».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net