Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 81

Al-A'raaf 7:81

الأعراف

إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ ٱلرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ ٱلنِّسَآءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ

Maana

Hakika nyinyi mnawaingilia wanaume kwa shahawa na mnawaacha wanawake? Bali nyinyi ni watu wapitilizao!"

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio mkwawacha wanawake? Kumbe nyinyi ni watu wafujaji! [81]

[81] Na jambo hilo ni kuwa mnawaendea wanaume kwa kuwatamani, na mnawawacha wanawake! Nyinyi kwa jambo hili inakuwa mnafanya fujo, na mmetoka nje ya maumbile, na mmefanya kitendo asicho fanya hata mnyama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nyinyi mnawaendea wanaume kwenye sehemu zao za nyuma, hali ya kuingiwa na matamanio ya kufanya hivyo, bila kujali uovu wake, huku mkiacha kile alichowahalalishia Allah Mtukufu kwa wake zenu. Bali nyinyi ni watu mliopita kiasi katika kukiuka mipaka ya Allah Mtukufu. Hakika kuwaendea wanaume badala ya wanawake ni miongoni mwa machafu ambayo yalianzishwa na kaumu ya Lût, na hawakutanguliwa na yoyote katika viumbe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net