Al-A'raaf 7:64
الأعراففَكَذَّبُوهُ فَأَنجَيْنَـٰهُ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥ فِى ٱلْفُلْكِ وَأَغْرَقْنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَآ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًا عَمِينَ
Basi walimkanusha. Nasi tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye katika jahazi. Na tukawazamisha wale waliozikanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu vipofu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi walimkanusha. Nasi tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika jahazi. Na tukawazamisha wale walio kanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu vipofu. [64]
[64] Lakini wao juu ya hoja hizo zilizo wazi wengi wao hawakuamini, bali walimkanusha. Kwa hivyo tukawateremshia adhabu ya kuwazamisha katika maji, na tukawaokoa wale walio amini katika jahazi alilo liunda kwa kuongozwa nasi. Na wakazama wale walio kanusha juu ya kuwapo hoja zilizo wazi, nao wakafanya inda wakawa hawaioni Haki kwa kuwa walipofuka wasiione.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi walimkanusha Nûḥ, tukamuokoa na wale walioamini pamoja na yeye katika jahazi, na tukawazamisha makafiri waliokanusha hoja zetu zilizowazi. Wao walikuwa vipofu wa nyoyo kwa kutoiona haki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net