Al-A'raaf 7:63
الأعرافأَوَعَجِبْتُمْ أَن جَآءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ وَلِتَتَّقُوا۟ وَلَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
Je, mnastaajabu kukujieni mawaidha yanayotoka kwa Mola Mlezi wenu kwa njia ya mtu ambaye ni mmoja wenu, ili akuonyeni na ili mumche Mungu, na ili mpate kurehemewa?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je, mnastaajabu kukujieni mawaidha yanayotoka kwa Mola Mlezi wenu kwa njia ya mtu aliye ni mmoja katika nyinyi, ili akuonyeni na ili mumchemngu, na ili mpate kurehemewa? [63]
[63] Mnanizulia kuwa nimepotea na kuwa nipo mbali na Haki? Na mnastaajabu kukujieni kumbusho kutokana na Mwenyezi Mungu aliye kuumbeni kwa ulimi wa mtu aliye kuja kwenu kukuonyeni adhabu pindi mkikanusha, na akakuiteni mwende kuufuata uwongofu, na kutengeza nyoyo, na kujiepusha na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kutaraji muwe katika rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu duniani na Akhera? Haifai kuwa mnastaajabu na mnakanusha juu ya kuwepo hoja zenye kuthibitisha Utume huu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je imewafanya nyinyi muone ajabu kwa kuwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ameteremsha kwenu yale ambayo yatawakumbusha mambo yenye kheri kwenu, kwa ulimi wa mtu miongoni mwenu, mnaoujua ukoo wake na ukweli wake, ili awaogopeshe adhabu ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na mateso Yake, na ili mujikinge na hasira Zake kwa kumuamini na kwa kutarajia kufaulu kupata rehema Zake na malipo Yake mema mengi?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net