Al-A'raaf 7:49
الأعرافأَهَـٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ ٱللَّهُ بِرَحْمَةٍ ۚ ٱدْخُلُوا۟ ٱلْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَآ أَنتُمْ تَحْزَنُونَ
Je, hawa ndio wale mliokuwa mkiwaapia kuwa Mwenyezi Mungu hatawafikishia rehema? Ingieni Peponi, hakuna hofu kwenu, wala hamtahuzunika!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je, hawa sio wale mlio kuwa mkiwaapia kuwa Mwenyezi Mungu hatawafikishia rehema. Ingieni Peponi, hapana khofu kwenu, wala hamtahuzunika! [49]
[49] Hao wanyonge mlio kuwa mkiwadharau, na mkaapa kuwa hayumkini Mwenyezi Mungu awateremshie rehema, kama kwamba nyinyi ndio mnao ishika rehema yake, wao wamekwisha ingia Peponi! Na Mola wao Mlezi atawaambia: Ingieni humo kwa amani. Hapana khofu juu yenu kwa jambo lolote litalo kupateni, wala hamtahuzunika kwa jambo mlilo likosa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je madhaifu na mafukara hawa, kati ya watu wa Peponi, ndio wale mlioapa huko duniani kwamba Allah Mtukufu Hatawakusanya Siku ya Kiyama Awatie kwenye rehema na Hatawaingiza Peponi? Ingieni Peponi, enyi watu wa Al-A‛rãf, hakika mmesamehewa; hamna tena hofu ya kupata adhabu ya Allah Mtukufu, wala hamtahuzunika juu ya hadhi za duniani zilizowapita.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net