Al-A'raaf 7:48
الأعرافوَنَادَىٰٓ أَصْحَـٰبُ ٱلْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُم بِسِيمَىٰهُمْ قَالُوا۟ مَآ أَغْنَىٰ عَنكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ
Na watu hao wa Minyanyukoni watawaita watu wanaowajua kwa alama zao. Watasema: Kujumuika kwenu hakukuwafaa kitu, wala hicho mlichokuwa mnakifanyia kiburi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hao watu wa Mnyanyukoni watawaita watu wanao wajua kwa alama zao. Watasema: Kujumuika kwenu hakukufaini kitu, wala hicho mlicho kuwa mnafanyia kiburi. [48]
[48] Na wale watu wa daraja za juu katika Pepo, nao ni Manabii, na Mas'iddiqina, watawaita walio kuwa wakiwajua kwa sifa zao katika watu wa Motoni, wakisema kwa kuwalaumu: Huko kujumuika kwenu kwa wingi, hakukufaini chochote, wala huko kupanda kiburi kuikataa Haki kwa kutegemea ujamaa wenu na utajiri wenu. Na hivi sasa mnawaona hawa, nini hali yao na nini hali yenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na watu walioko Al-A‛rãf watawaita wanaume, miongoni mwa viongozi wa makafiri waliomo motoni, wanaowajua kwa alama zao fulani zinazowatenganisha wawaambie, «Hayakuwafaa chochote mali mliokuwa mkiyakusanya ulimwenguni wala watu; pia hakikuwafaa kiburi chenu kilichowafanya nyinyi msimuamini Allah Mtukufu na msiikubali haki».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net