Al-A'raaf 7:18
الأعرافقَالَ ٱخْرُجْ مِنْهَا مَذْءُومًا مَّدْحُورًا ۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنْهُمْ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمْ أَجْمَعِينَ
Akasema: Toka humo ilhali umefedheheshwa, umefukuzwa. Hakuna shaka atakayekufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote [18]
[18] Mwenyezi Mungu akazidi kuudhika, akamwambia: Toka kwenye makao ya ukarimu wangu, wewe ulio hizika kwa kiburi chako na uasi wako, na khatima yako ni kuhiliki tu! Na ninaapa nitaijaza Jahannamu kwa wewe na hao wana wa Adam watao kufuata nyote pamoja!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, (Aliyetukuka,) Akasema, kumwambia Iblisi, «Toka Peponi ukiwa umechukiwa na umefukuzwa. Nitaujaza Moto wa Jahanamu kwa kukuingiza wewe humo na binadamu wote watakaokufuata».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net