Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 17

Al-A'raaf 7:17

الأعراف

ثُمَّ لَـَٔاتِيَنَّهُم مِّنۢ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَـٰنِهِمْ وَعَن شَمَآئِلِهِمْ ۖ وَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَـٰكِرِينَ

Maana

Kisha nitawajia kwa mbele yao na kwa nyuma yao na kuliani kwao kwote na kushotoni kwao kwote. Wala hutawakuta wengi wao ni wenye shukrani.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani. [17]

[17] Na ninaapa, nitawatokelea mbele yao, na nyuma yao, na kuliani kwao, na kushotoni kwao, na kila upande ninao weza, nikitafuta kila kipengee cha kughafilika kwao au udhaifu wao, nipate kuwapotosha, hata wasiwe wengi wao wanao kuamini Wewe, kwa kuto shukuru neema yako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha nitawajia kutoka pande zote na pambizo niwazuie wasiifuate haki, niwapambie batili, niwafanye wavutike na dunia na niwatie shaka kuhusu Akhera. Na hutawapata wengi wa wanadamu ni wenye kukushukuru wewe kwa neema zako.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net