Al-A'raaf 7:133
الأعراففَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ ٱلطُّوفَانَ وَٱلْجَرَادَ وَٱلْقُمَّلَ وَٱلضَّفَادِعَ وَٱلدَّمَ ءَايَـٰتٍ مُّفَصَّلَـٰتٍ فَٱسْتَكْبَرُوا۟ وَكَانُوا۟ قَوْمًا مُّجْرِمِينَ
Basi tukawatumia tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu, ziwe ni Ishara za kina. Lakini wakatakabari, na wakawa kaumu wahalifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi tukawapelekea tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu, kuwa ni Ishara mbali mbali. Nao wakapanda kiburi, na wakawa watu wakosefu. [133]
[133] Basi Mwenyezi Mungu aliwateremshia masaibu na balaa zaidi, kama tufani lilio funika mwahala mwao, na nzige walio kula kila mmea na mti ulio bakia, na chawa, yaani vijidudu vinavyo haribu matunda na kuteketeza wanyama na mimea. na vyura vilivyo enea vikafanya maisha yao dhiki, na vikachafua kila pahala, na damu iliyo sabibisha maradhi mengi, kama kupasuka mishipa ya damu katika mwili, na damu inayo najisisha kila pahala ikasabibisha presha, au kupasuka ikaleta kiharusi na kupooza, na kutokwa na mkojo wa damu kwa sababu ya kichocho na mfano wake, au ikawa inachanganyika na maji yao wanayo hitajia kunywa au kupikia. Mwenyezi Mungu aliwapatiliza na Ishara hizi zote zilio wazi! Nao wasiathirike, nyoyo zao zikabaki kuwa ngumu, na wenye kutakabari hawataki Imani wala kurejea kwenye Haki. Walikuwa watu walio bobea kwenye madhambi na ukosefu, kama ilivyo ada yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tukawapelekea wao mafuriko yenye kumaliza yaliyozamisha mazao na matunda; tukapeleka nzige wakazila nafaka zao, matunda yao, milango yao, sakafu zao na nguo zao; na tukapeleka chawa wanaoharibu matunda na kumaliza wanyama na mimea; tukapeleka vyura wakajaa kwenye vyombo vyao na vyakula vyao na malazi yao; na pia tukapeleka damu, ikawa mito yao na visima vyao vimegeuka damu, wasipate maji safi ya kunywa. Hii ni miujiza kati ya miujiza ya Allah Mtukufu, hakuna aiwezae isipokuwa Yeye, baadhi yake imetengwa na mingine. Pamoja na haya yote, watu wa Fir‛awn walijiona watukufu, wakafanya kiburi kwa kukataa kumuamini Allah Mtukufu, wakawa ni watu Wanaotenda mambo Anayoyakataza Allah Mtukufu ya maasia na uhalifu kwa, ujeuri na uasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net