Al-A'raaf 7:132
الأعرافوَقَالُوا۟ مَهْمَا تَأْتِنَا بِهِۦ مِنْ ءَايَةٍ لِّتَسْحَرَنَا بِهَا فَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ
Na walisema, "Hata ukitujia na Ishara zozote zile kutufanyia uchawi kwazo, basi sisi hatutakuamini."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakisema: Hata ukituletea Ishara yoyote kutuzuga hatuto kuamini. [132]
[132] Na kwa hii fikra mbovu waliyo nayo wakaendelea na upinzani. Walisema walipo ona miujiza ya Musa: Wewe hata ukituletea kila namna ya Ishara zinazo onyesha ukweli wa wito wako, ili kutuachisha dini yetu, na tusiwafanye watumwa watu wako, sisi hatukusadiki wala hatukufuati.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watu wa Fir‛awn wakasema kumwambia Mûsã, «Alama yoyote utakayotuletea, na dalili na hoja zozote utakazotusimamishia ili utuepushe na dini ya Fir‛awn tuliyonayo, sisi si wenye kukuamini»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net