Al-A'raaf 7:130
الأعرافوَلَقَدْ أَخَذْنَآ ءَالَ فِرْعَوْنَ بِٱلسِّنِينَ وَنَقْصٍ مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ
Na hakika tuliwachukua watu wa Firauni kwa miaka (ya ukame), na kwa upungufu katika mazao, huenda wakakumbuka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika tuliwaadhibu watu wa Firauni kwa miyaka (ya ukame) na kwa upungufu wa mazao, ili wapate kukumbuka. [130]
[130] Na hakika Sisi tuliwaadhibu Firauni na watu wake kwa ukame, na dhiki ya maisha, na upungufu wa matunda na mazao na miti, kwa kutaraji kuwa watazindukana wautambue unyonge wao, na kushindwa ufalme wao wa jeuri mbele ya nguvu za Mwenyezi Mungu, wapate kuwaidhika na waache kuwadhulumu Wana wa Israili, na wauitikie wito wa Musa a.s. Kwani mtindo wa shida ni kuzuia kujidanganya, na kutengeza tabia, na kuzielekeza nafsi ziikubali Haki, na kumridhi Mola Mlezi wa viumbe vyote, na kumnyenyekea Yeye tu, si mwenginewe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika tulimpa Fir‛awn na watu wake mtihani wa chaka na ukame na upungufu wa matunda yao na nafaka zao ili wakumbuke na wakome, waache upotevu wao na wakimbilie kwa Mola wao kwa kutubia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net