Al-A'raaf 7:129
الأعرافقَالُوٓا۟ أُوذِينَا مِن قَبْلِ أَن تَأْتِيَنَا وَمِنۢ بَعْدِ مَا جِئْتَنَا ۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ
Wakasema: Tumeudhiwa kabla wewe kutujia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamuangamiza adui wenu, na akawafanya nyinyi ndio wa kufuatia kushika ardhi, ili atazame mtakavyokujatenda nyinyi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamhiliki adui wenu, na akakufanyeni nyinyi ndio wa kufuatia kushika nchi, ili atazame mtavyo kuja tenda nyinyi. [129]
[129] Wakasema wale watu kwa huzuni na unyonge: Sisi tulipata maudhi zamani kutoka kwa Firauni kabla hujatujia, na hivi sasa tena baada ya kuja kwako. Musa akawafungulia mlango wa matarajio mema kwa kuwaambia: Hakika linalo tarajiwa kwa fadhila za Mola wenu Mlezi ni kumteketeza adui yenu, aliye kufanyeni watumwa na akakuteseni kwa dhulma yake, na akujaalieni nyinyi ndio wa kuimiliki ardhi aliyo kuahidini. Yeye Subhanahu, Aliye takasika, anayajua mnayo yatenda baada ya kukuwekeni huku. Je, mtaishukuru neema au mtaikufuru? Na mtatenda mema katika nchi au mtafanya fisadi? Hayo ili apate kukulipeni duniani na Akhera kwa mujibu wa mtendayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walisema watu wa Mûsã, miongoni mwa Wana wa Isrãîl, kumwambia Nabii wao Mûsã, «Tulisumbuliwa na tukaudhiwa na nguvu za Fir‛awn na watu wake, kwa kuuawa watoto wetu wa kiume na kuachiliwa wanawake wetu, kabla hujatujia na baada ya kutujia.» Mûsã akawaambia, «Huenda Mola wenu Akamuangamiza adui yenu, Fir‛awn na watu wake, na Awaweke nyinyi katika ardhi yao badala yao, baada ya kuangamia kwao, Aangalie namna mtakavyofanya: mtashukuru au mtakufuru?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net