Al-A'raaf 7:113
الأعرافوَجَآءَ ٱلسَّحَرَةُ فِرْعَوْنَ قَالُوٓا۟ إِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ ٱلْغَـٰلِبِينَ
Na wachawi wakamjia Firauni, wakasema: Hakika tutapata ujira ikiwa tutakuwa sisi ndio washindi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakaja wachawi kwa Firauni, wakasema: Hakika tutapata ujira ikiwa tutashinda. [113]
[113] Basi wakaja kwa Firauni wachawi walio kusanywa na askari wake. Nao wakasema: Hapana shaka nasi tutapata malipo makubwa yanayo lingana na hili linalo takikana kwetu, ikiwa sisi tutamshinda Musa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wachawi wakamjia Fir‛awn wakasema, «Je, tutakuwa na zawadi na mali tukimshinda Mûsã?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net