Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 106

Al-A'raaf 7:106

الأعراف

قَالَ إِن كُنتَ جِئْتَ بِـَٔايَةٍ فَأْتِ بِهَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ

Maana

Akasema (Firauni), "Ikiwa umekuja na ishara yoyote, basi ilete ikiwa wewe ni katika wakweli."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema Firauni: Ikiwa umekuja na Ishara, basi ilete ukiwa ni katika wasemao kweli. [106]

[106] Firauni akamwambia Musa: Ikiwa umekuja na Ishara (muujiza) kutokana na huyo aliye kutuma, basi nionyeshe kama wewe ni katika watu wakweli wanalo lishika neno la haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Fir‛awn alisema kumwambia Mûsã, «Ukiwa umekuja na alama, kama unavyodai, basi niletee na uihudhurishe mbele yangu, ili madai yako yawe ya sawa na ukweli wako uthibiti, iwapo wewe ni mkweli katika madai yako kuwa wewe ni mjumbe wa Mola wa viumbe».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net