Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 7 · Aya ya 105

Al-A'raaf 7:105

الأعراف

حَقِيقٌ عَلَىٰٓ أَن لَّآ أَقُولَ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلْحَقَّ ۚ قَدْ جِئْتُكُم بِبَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَرْسِلْ مَعِىَ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ

Maana

Inastahiki zaidi juu yangu kwamba nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu. Hakika nimewajia na Ishara za waziwazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi waachilie pamoja nami Wana wa Israili."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Inafaa nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila lilio la Haki. Nami hakika nimekujieni na dalili waziwazi kutokana na Mola Mlezi wenu. Basi waache Wana wa Israili wende nami. [105]

[105] Na mimi pupa yangu ni kumsemea kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na nimekujieni na Ishara yenye shani kubwa, yenye hoja iliyo dhaahiri katika kubainisha Haki niliyo kuja nayo. Basi waachilie waje nami Wana wa Israili, na uwatoe kwenye utumwa wa kahari yako, wende nami kwenye nchi nyengine isiyo kuwa yako, na huko wapate kumuabudu Mola Mlezi wao na wako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Nastahili nisiseme kuhusu Allah Mtukufu isipokuwa ukweli na inapasa kwangu nijilazimishe nayo. Nimewajia na dalili na hoja zenye ushindi kutoka kwa Mola wenu juu ya ukweli wa yale ninayowatajia. Basi waachilie, ewe Fir‛awn, Wana wa Isrãîl pamoja na mimi kutoka kwenye kifungo chako na ukandamizaji wako, na wape uhuru wa kumuabudu Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-A'raaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net