Al-Mulk 67:9
الملكقَالُوا۟ بَلَىٰ قَدْ جَآءَنَا نَذِيرٌ فَكَذَّبْنَا وَقُلْنَا مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ مِن شَىْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ كَبِيرٍ
Watasema: 'Kwani! Ametujia mwonyaji, lakini tulimkadhibisha, na tukasema: 'Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamumo ila katika upotovu mkubwa!''
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Watasema: Kwani! Ametujia mwonyaji, lakini tulimkadhibisha, na tukasema: Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamumo ila katika upotovu mkubwa! [9]
[9] Na wao watajibu: Ametujia mwonyaji, lakini sisi tulimkanusha tukamwambia mwongo, na tukasema: Mwenyezi Mungu hakukuteremshia chochote wewe wala Mitume wenginewe. Nyinyi mnao dai Utume si chochote ila ni watu walio potoka, na mko mbali na haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watawajibu kwa kusema, Ndio! Tumejiwa na Mjumbe anayetoka kwa Allah Mtukufu, akatuonya na tukamkanusha na tukasema kuhusu miujiza aliyokuja nayo: Allah Mtukufu hakumteremshia binadamu kitu chochote. nyinyi si kingine, (enyi Mitume), isipokuwa mmeenda mbali na haki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net