Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 67 · Aya ya 8

Al-Mulk 67:8

الملك

تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ ٱلْغَيْظِ ۖ كُلَّمَآ أُلْقِىَ فِيهَا فَوْجٌ سَأَلَهُمْ خَزَنَتُهَآ أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَذِيرٌ

Maana

Inakaribia kupasuka kwa hasira. Kila mara likitupwa kundi humo, walinzi wake huwauliza: 'Kwani hakukujieni mwonyaji?'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Inakaribia kupasuka kwa hasira. Kila mara likitupwa kundi humo walinzi wake huwauliza: Kwani hakukujieni mwonyaji? [8]

[8] Unakaribia kukatika na kutawanyika kwa wingi wa kuwaghadhibikia. Kila likitumbukizwa kundi mojapo kati yao walinzi wake huwauliza kwa kuwakejeli: Kwani hakukujieni Mtume kukuhadharisheni na mkutano wa siku hii ya leo?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Unakaribia huo moto wa Jahanamu kupasuka kwa ukali wa hasira ulizonazo juu ya wakanushaji. Kila linapotiwa humo kundi la watu, wale wawakilishi wa kusimamia mambo ya huo moto wa Jahanamu wanawauliza kwa njia ya kuwalaumu na kuwakaripia: Je kwani hakuwajia, huko duniani, mjumbe wa kuwatahadharisha na adhabu hii ambayo nyinyi mmo ndani yake?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mulk

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net