Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 67 · Aya ya 22

Al-Mulk 67:22

الملك

أَفَمَن يَمْشِى مُكِبًّا عَلَىٰ وَجْهِهِۦٓ أَهْدَىٰٓ أَمَّن يَمْشِى سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Maana

Je, anayekwenda akisinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi, au yule anayekwenda sawasawa katika Njia iliyonyooka?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Anaye kwenda akisinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi, au yule anaye kwenda sawasawa katika Njia Iliyo Nyooka? [22]

[22] Je! Hali itageuka? Mwenye kwenda akijikwaa na kusinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi katika mwendo wake, au yule anaye tembea sawasawa kwenye njia isiyo kwenda upogo?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je huyu anayetembea akiwa kichwa chake kimeinama hajui pa kuelekea wala namna ya kutembea ndiye aliyeko kwenye uongofu zaidi au ni yule anayetembea sawasawa? akiwa na kimo kilicholingana, aliye mzima, afuataye njia iliyo ya wazi isiyokuwa na kupinda? Na huu ni mfano Allah Mtukufu Amempigia kafiri na muumini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mulk

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net