Al-Munaafiqoon 63:7
المنافقونهُمُ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُوا۟ عَلَىٰ مَنْ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّوا۟ ۗ وَلِلَّهِ خَزَآئِنُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَلَـٰكِنَّ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ
Hao ndio wanaosema: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, ili waondokelee mbali! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio wanao sema: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, ili waondokelee mbali! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye khazina za mbingu na ardhi, lakini wanaafiki hawafahamu. [7]
[7] Hao wanaafiki ndio wanao waambia watu wa Madina: Msitoe chochote kuwapa hao Waumini walio na Mtume wa Mwenyezi Mungu ili wapate kumwacha! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye khazina zote za mbinguni na duniani, na riziki zote ziliomo humo. Lakini wanaafiki hawajui hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanafiki hawa ndio wanaosema kuwaambia watu wa Madina, «Msitoe kuwasaidia Maswahaba wa Mtume wa Allah Mtukufu waliohama mpaka wajiepushe naye.» Ni za Allah Mtukufu, Peke Yake, hazina za mbinguni na ardhini na vilivyomo humo miongoni mwa riziki, Humpa Anayemtaka na Humnyima Anayemtaka, lakini wanafiki hawaelewi kwamba riziki inatoka kwa Allah Mtukufu kwa ujinga wao wa kutomjua, kutakasika na kila upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net