Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 62 · Aya ya 8

Al-Jumu'a 62:8

الجمعة

قُلْ إِنَّ ٱلْمَوْتَ ٱلَّذِى تَفِرُّونَ مِنْهُ فَإِنَّهُۥ مُلَـٰقِيكُمْ ۖ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَـٰلِمِ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Maana

Sema: Hayo mauti mnayoyakimbia, bila ya shaka yatakukuteni. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kujua zaidi yaliyofichikana na yanayoonekana. Hapo atakwambieni mliyokuwa mkiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Hayo mauti mnayo yakimbia, bila ya shaka yatakukuteni. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda. [8]

[8] Sema: Hayo mauti mnayo yakimbia hamwezi kuyakimbia, bila ya shaka yatakukuteni tu. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kujua ya siri na ya dhaahiri. Na Yeye atakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, «Kwa kweli mauti mnayoyakimbia hayakimbiliki, kwani ni yenye kuwajia wakati wenu wa kufa utakapofika, kisha Siku ya kufufuliwa mtarudishwa kwa Allah Mtukufu, mjuzi wa yale yaliyofichika na yanayoonekana, na hapo Atawapasha habari ya matendo yenu na Atawalipa nyinyi kwa hayo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jumu'a

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net