Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 62 · Aya ya 7

Al-Jumu'a 62:7

الجمعة

وَلَا يَتَمَنَّوْنَهُۥٓ أَبَدًۢا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyokwisha yatanguliza mikono yao. Na Mwenyezi Mungu anawajua mno madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyo kwisha yatanguliza mikono yao. Na Mwenyezi Mungu anawajua walio dhulumu. [7]

[7] Mwenyezi Mungu anasema: Wala Mayahudi hawatamani mauti milele kwa sababu ya ukafiri na vitendo viovu walio kwisha vitenda. Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema walio dhulumu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wala hawa Mayahudi hawatatamani kifo kabisa kwa vile wanavyoyapenda maisha ya duniani kuliko Akhera, na kwa kuogopa kuteswa na Allah Mtukufu, kwa sababu ya yale waliyoyatanguliza ya ukafiri na matendo maovu. Na Allah Mtukufu Anawajua mno madhalimu, hakifichiki Kwake chochote cha udhalimu wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jumu'a

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net