Al-Mumtahana 60:9
الممتحنةإِنَّمَا يَنْهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِينَ قَـٰتَلُوكُمْ فِى ٱلدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَـٰرِكُمْ وَظَـٰهَرُوا۟ عَلَىٰٓ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ
Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki wa kusaidiana nao, na wale waliokupigeni vita kwa sababu ya dini, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanaowafanya hao marafiki, basi hao ndio madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu. [9]
[9] Ila Mwenyezi Mungu anakukatazeni wale walio kupigeni vita katika Dini ili kukuzuieni nayo, na wakakulazimisheni kutoka majumbani kwenu na nchi yenu, na wakasaidia katika kukutoeni huko, msiwafanye hao kuwa ndio wenzenu wa kusaidiana nao. Na wenye kuwafanya hao ndio wasaidizi wao, basi hao ndio wenye kujidhulumu nafsi zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Allah Mtukufu Anawakataza, kuhusu wale waliowapiga vita kwa ajili ya dini na wakawatoa majumbani mwenu na wakawasaidia makafiri kuwatoa nyinyi, kufanya urafiki nao kwa kusaidiana na kupendana. Na yoyote atakayewafanya wao kuwa wasaidizi wake na vipenzi vyake dhidi ya Waumini, basi hao ndio madhalimu wa nafsi zao, wenye kutoka nje ya mipaka ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net