Al-Mumtahana 60:10
الممتحنةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا جَآءَكُمُ ٱلْمُؤْمِنَـٰتُ مُهَـٰجِرَٰتٍ فَٱمْتَحِنُوهُنَّ ۖ ٱللَّهُ أَعْلَمُ بِإِيمَـٰنِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَـٰتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى ٱلْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ ۖ وَءَاتُوهُم مَّآ أَنفَقُوا۟ ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَآ ءَاتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۚ وَلَا تُمْسِكُوا۟ بِعِصَمِ ٱلْكَوَافِرِ وَسْـَٔلُوا۟ مَآ أَنفَقْتُمْ وَلْيَسْـَٔلُوا۟ مَآ أَنفَقُوا۟ ۚ ذَٰلِكُمْ حُكْمُ ٱللَّهِ ۖ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ ۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
Enyi mlioamini! Wakikujilieni wanawake Waumini waliohama, basi wafanyieni mtihani - Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao. Mkiwa mnawajua kuwa ni Waumini, basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini. Na wapeni hao wanaume mahari waliotoa. Wala hapana makosa kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu. Na takeni mlichokitoa, na wao watake walichokitoa. Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu anayokuhukumuni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mno, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Wakikujilieni wanawake Waumini walio hama, basi wafanyieni mtihani - Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao. Mkiwa mnawajua kuwa ni Waumini basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini. Na wapeni hao wanaume mahari walio toa. Wala hapana makosa kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu. Na takeni mlicho kitoa, na wao watake walicho kitoa. Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu anayo kuhukumuni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima. [10]
[10] Enyi mlio amini! Wakikujieni wanawake Waumini walio hama kukimbia nchi ya ukafiri, basi wachungueni ili mpate kujua ukweli wa Imani yao. Mwenyezi Mungu anajua zaidi ukweli wa Imani yao. Mkiwaona kama ni Waumini, basi msiwarudishe kwa waume zao makafiri. Wanawake Waumini si halali kwa makafiri, wala wanaume makafiri si halali kwa wanawake Waumini. Na wapeni waume wa kikafiri mahari waliyo yatoa kwa wake zao walio hamia kwenu. Wala hapana ubaya kwenu kuwaoa wanawake hao walio hamia kwenu mkiwapa mahari yao. Wala msiwazuie kwa kifungo cha ndoa wanawake makafiri walio bakia katika mji wa ukafiri au walio fungamana nao. Na takeni kwa makafiri mahari mliyo yatoa kwa wenye kufungamana na mji wa ukafiri. Na wao hao watake kulipwa walicho toa kuwapa wake zao walio hama wakaja kwenu. Hukumu hiyo ni kwa mujibu wa sharia ya Mwenyezi Mungu, anayo kufafanulieni. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema maslaha ya waja wake, ni Mwenye hikima katika kutoa sharia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini (Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo)! Wakiwajia wanawake Waumini wakiwa wamehama kutoka nchi ya ukafiri kuja kwenye nchi ya Uislamu, wafanyieni mtihani, ili mjue ukweli wa Imani yao, Allah Mtukufu Ndiye Mjuzi zaidi wa Imani yao. Mkiwajua kuwa ni Waumini kulingana na alama na ushahidi utakaowadhihirikia, basi msiwarudishe kwa waume wao makafiri. Kwani wanawake Waumini si halali waolewe na makafiri, na makafiri si halali wawaoe wanawake Waumini. Nawapeni waume wa wale wanawake waliosilimu mahari waliotoa kuwapa hao wanawake. Na si dhambi kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Na msishikilie kuendelea na ndoa za wake wenu waliokufuru. Na takeni kwa washirikina mrudishiwe mahari mliotoa kuwapa wanawake wenu walioritadi na wakaungana na hao washirikina. Na wao watake kurudishiwa mahari waliotoa kwa wanawake wao waliosilimu na wakaungana na nyinyi. Hukumu hii iliyotajwa katika aya hii ni hukumu ya Allah Mtukufu Anahukumu baina yenu, basi msiende kinyume nayo. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi, hakuna kitu chochote kinachofichika Kwake, ni Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net