Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 59 · Aya ya 21

Al-Hashr 59:21

الحشر

لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُۥ خَـٰشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ ٱللَّهِ ۚ وَتِلْكَ ٱلْأَمْثَـٰلُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ

Maana

Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur-ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeliuona ukinyenyekea, ukipasuka kwa kumhofu Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur'ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri. [21]

[21] Lau tungeli iteremsha hii Qur'ani juu ya mlima wenye nguvu basi ungeli uona huo mlima, juu ya nguvu zake, unanyenyekea na unapasuka kwa kumwogopa Mwenyezi Mungu. Na hiyo ni mifano tunawaelezea watu ili wapate kuzingatia matokeo ya mambo yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lau tungeiteremsha hii Qur’ani juu ya jabali (moja miongoni mwa majabali), na likaelewa yaliyo ndani yake ya ahadi ya malipo mema kwa watu wema na malipo mabaya kwa watu wabaya, ugeliona, pamoja na nguvu zake, ugumu wake na ukuu wake, limenyenyekea, limejidhalilisha na limepasukapasuka kwa kumuogopa Allah Mtukufu Aliyetukuka. Na hiyo ni mifano tunawapigia watu na kuwabainishia, ili wafikirie juu ya uwezo wa Allah Mtukufu na ukubwa Wake. Katika aya hii pana kuhimiza kuizingatia Qur’ani na kujifahamisha maana yake na kuitumia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hashr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net