Al-Hashr 59:20
الحشرلَا يَسْتَوِىٓ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ وَأَصْحَـٰبُ ٱلْجَنَّةِ ۚ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَنَّةِ هُمُ ٱلْفَآئِزُونَ
Hawawi sawa watu wa Motoni na watu wa Bustani ya mbinguni. Watu wa Bustani ya mbinguni ndio wenye kufuzu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hawawi sawa watu wa Motoni na watu wa Peponi. Watu wa Peponi ndio wenye kufuzu. [20]
[20] Hawawi sawa watu wa Motoni wanao teswa, na watu wa Peponi wanao neemeshwa. Watu wa Peponi peke yao ndio wenye kufuzu kwa kila walipendalo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawalingani watu wa Motoni wanaoadhibiwa na watu wa Peponi wanaostareheshwa. Watu wa Peponi ndio wenye kupata kila kinachotakiwa, ndio wenye kuokoka na kila kinachochukiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net