Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 58 · Aya ya 19

Al-Mujaadila 58:19

المجادلة

ٱسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ فَأَنسَىٰهُمْ ذِكْرَ ٱللَّهِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ حِزْبُ ٱلشَّيْطَـٰنِ ۚ أَلَآ إِنَّ حِزْبَ ٱلشَّيْطَـٰنِ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ

Maana

Shetani amewatawala na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Sikilizeni, hakika kundi la Shetani ndilo lenye kuhasirika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Shetani amewatawala na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Kweli hakika kundi la Shetani ndilo lenye kukhasirika. [19]

[19] Shetani amewatawala na amewasahaulisha kumdhukuru Mwenyezi Mungu na kuukumbuka utukufu wake. Hao ndio kundi la Shetani. Ama kweli, hakika kundi la Shetani ndilo lilio fikilia mwisho wa kukhasiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao Shetani aliwaghilibu na akawatawala mpaka wakaacha amri za Allah Mtukufu na kufanya matendo ya utiifu Kwake. Hao ni kundi la Shetani na wafuasi wake. Jua utanabahi kwamba watu wa kundi la Shetani ndio wenye kupata hasara duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Mujaadila

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net